Mambo ya Msingi kuhusu Majadiliano

Bofya hapa ili kupakua hii kama PDF inayoweza kuchapishwa.

Majadiliano ya masilahi ya kikazi ni nini?

Majadiliano ya masilahi kikazi ni mchakato wa kisheria wa kujadili makubaliano kati ya muungano wa wafanyakazi na mwajiri kuhusu sheria na masharti ya ajira, kama vile mishahara, saa za kazi, likizo zinazolipwa, marupurupu, uhakikisho wa ajira, na ulinzi dhidi ya kutendewa visivyo au kufutwa.

Majadiliano ya masilahi ya kikazi kwa kawaida husababisha kuandikwa kwa mkataba unaoelezea sheria na masharti ya ajira. 

Kwa nini ni muhimu kuwe na mkataba?

Mkataba wetu unaelezea kwa uwazi sheria na masharti ya ajira yetu kwa wajumbe walio kwenye majadiliano na usimamizi na unatuhakikishia kuwa tuna utaratibu wa kusuluhisha malalamiko na kuleta mapatano unaotulinda iwapo kampuni itakiuka mkataba wetu, hali inayoturuhusu kumfanya mwajiri wetu awajibike. 

Hii ina maana kwamba wasimamizi hawawezi kuamua kivyao kupunguza mishahara na marupurupu, kuwafuta wafanyakazi, kupendelea watu fulani, kubadilisha ratiba na likizo au kufanya mabadiliko mengine yanayoweza kutudhuru. Pia hutupatia njia mwafaka ya kupinga hatua ambazo mwajiri huchukua.

Je, muda wa mikataba yetu utakwisha lini?

Mikataba inayohusu wafanyakazi wanaoshughulikia bidhaa moto (idara ya mashine za otomatiki) na wafanyakazi wanaoshughulikia bidhaa baridi (idara ya uzalishaji na matengenezo) itaisha tarehe 31 Machi 2023. 

Mkataba unaohusu watengenezaji wa kalibu utaisha tarehe 31 Agosti 2023.

Majadiliano haya hushughulikia Miungano gani ya Kimaeneo na maeneo gani ya kazini?

Majadiliano na Anchor Glass hushughulikia takribani wanachama 1,500 katika maeneo sita kote nchini.

  • Locals 104M, 180M, 135T katika Elmira Heights, N.Y.
  • Locals 48M, 145 katika Henryetta, Okla.
  • Locals 91M, 38 katika Jacksonville, Fla.
  • Locals 42M, 138 katika Lawrenceburg, Ind.
  • Locals 129M, 133T katika Shakopee, Minn.
  • Locals 234M, 3T katika Warner Robins, Ga.

Tunawezaje kupata mkataba bora kwenye Anchor?

Kampuni hii “haitatupatia” chochote. Haijawahi na haitawahi.

Jinsi walivyo waajiri wengi, Anchor huboresha mishahara, marupurupu au mazingira ya kazi wakati tu inalazimishwa kufanya hivyo. Tutahitaji kuwaonyesha wasimamizi umoja na azma yetu ili kupinga majaribio ya kampuni ya kuweka makubaliano yasiyofaa na kufikia malengo yetu wakati wa majadiliano. 

Ni aina gani ya mapendekezo hujadiliwa katika majadiliano haya?

Wahusika wanaweza kujadili suala lolote linaloathiri eneo la kazi. Kwa kawaida, mapendekezo ya mkataba hubainishwa katika mojawapo ya aina hizi mbili:

  1. Mapendekezo ya kiuchumi, kama vile mishahara, likizo inayolipwa, bima ya afya, pensheni au marupurupu ya ugonjwa na ajali, na
  2. Mambo yasiyo ya kiuchumi, kama vile viwango vya usalama, ukuu, na utaratibu wa kusuluhisha malalamiko na kuleta upatanishi.

Waakilishi wa miungano ya kimaeneo na wenzao walio katika usimamizi ambao wanafahamu mchakato huu zaidi watajadili na kutatua masuala mahususi kulingana na kiwanda. Mara nyingi hatua hizi hujulikana kama “makubaliano ya kimaeneo” na huandikwa na kuwekwa saini na Muungano wa Kimaeneo na wasimamizi wa kiwanda cha kimaeneo.

Majadiliano haya hufanyikaje?

Majadiliano hufanyika kwenye meza ya majadiliano ambapo waakilishi wa mwajiri na wa muuungano wetu hukutana ili kujadili mapendekezo yanayoshughulikia masuala yetu.

Wajumbe wa pande zote mbili (hukutana kivyao), hutoa mapendekezo ya kukanusha, hujaribu dhana na kutafuta njia za kutatua tofauti.

Hakuna anayeridhika kwa asimilia 100 na mapendekezo yanayotolewa kati ya kampuni na muungano, lakini usimamizi unapofahamu kuwa tumeungana, kuna uwezekano mkubwa wa kufikia mkataba wa haki.

Ni nani hujadili mikataba kwa niaba yetu?

Katika majadiliano ya makubaliano makuu ya wafanyakazi wanaoshughulikia bidhaa moto na wanaoshughulikia bidhaa baridi, wajumbe kutoka kwenye kila Muungano wa Kimaneo, uongozi wa USW na wafanyakazi wenye uzoefu wote watahusika. Claude Beaudin atakuwa mwenyekiti na atasimamia majadiliano ya mikataba hii.

Majadiliano ya makubaliano makuu ya watengenezaji kalibu huendeshwa na Kamati ya Majadiliano ya Utengenezaji wa Kalibu, ambayo wajumbe wake huchaguliwa kutoka ndani ya kampuni na katika sekta. Rob Witherell kutoka idara ya Majadiliano ya Masilahi ya Kikazi ya USW ataongoza majadiliano haya.

Ninawezaje kujua kinachoendelea kwenye meza ya majadiliano?

Unaweza kupokea ujumbe wa SMS kwenye simu yako ya mkononi kama ungependa kupokea habari za hivi punde kutoka kwenye majadiliano.

Ili ujisajili, tuma neno Anchor kwa nambari ya simu 47486

Ada za SMS au data zinaweza kutozwa. Unaweza kujiondoa kwa kutuma neno “stop” kwa 47486.